Meneja wa Mabigwa wa Soka nchini Hispania Real Madrid Carlo Ancelotti amethibitisha kuwa Shirikisho la Soka nchini Brazil ‘CBF’ limedhamiriakufanya naye kazi kama Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya nchi hiyo, lakini amesisitiza nia yake ya kubakia Real Madrid.

Brazil imekuwa bila kocha mkuu tangu Tite alipoondoka baada ya Fainali za Kombe la Dunia 2022 na ripoti mbalimbali zinadai Ancelotti ndiye anayewindwa kila kukicha.

Mshambuliaji wa Madrid, Vinicius Jr juma lililopita alisema “anaamini” kocha wa klabu yake anataka kuchukua kazi kwa ‘Selecao’ hao na Ancelotti anafurahishwa na nia hiyo.

“Ukweli ni kwamba timu ya taifa ya Brazil inanitaka, naipenda hiyo, inasisimua,” Ancelotti  aliwaambia wanahabari kabla ya mchezo wa Madrid dhidi ya Real Valladolid.

“Kutoka hapo, ni lazima mkataba wangu uheshimiwe, kwa hiyo ni mapema mno kusema lolote, japo ninahitaji kuendelea kufanya kazi hapa.”

Ancelotti mwenye umri wa miaka 63, ana mkataba na Real Madrid hadi mwaka 2024.

Alirejea katika klabu hiyo kwa kipindi cha pili cha kuinoa 2022 na kuwaongoza ‘Los Blancos’ kutwaa La Liga na Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita.

Mwaka huu, Madrid wako nyuma kwa alama 12 dhidi ya vinara FC Barcelona kwenye La Liga, lakini wamesalia kwenye Ligi ya Mabinga wa Ulaya na Kombe la Mfalme.

Mustakabali Meneja huyo kutoka nchini Italia wake unatarajiwa kuhusishwa na jinsi Madrid wanavyofanya katika mashindano hayo mawili, ingawa amesisitiza kwamba anataka kubaki Santiago Bernabeu.

Serikali yafufua ujenzi Stendi mpya ya Mabasi Kyakailabwa
Serikali kuliimarisha jiji la Dodoma vivutio vya utalii