Scolastica Msewa, Chalinze – Pwani.
Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Nchini – CBT, Brigedia General Mstaafu, Aloyce Mwanjile amesema ataanzisha shamba darasa la Korosho katika Shule ya Sekondari ya Kimange Chalinze, ili ijiimarishe kiuchumi na kutoa elimu ya Kilimo cha zao hilo kwa Wanafunzi Mkoa wa Pwani.
General Mwanjile ameyasema hayo wakati akihutubia mahafari ya Kumi ya Shule ya Sekondari ya Kata ya Kimange Chalinze, Pwani ambapo na kudai kuwa Kilimo cha korosho ni miongoni mwa mazao yanayoweza kuwakwamua Vijana kiuchumi, hivyo aliwasisitiza wahitimu kufanya kazi kwa bidii hususani katika kilimo cha Korosho.
Amesema “tuingie mkataba na Walimu, niwaombe kuanzia Leo Mimi ni rafiki wa hii Shule Mimi baada ya kustaafu jeshi nimekuwa mkulima wa korosho na bahati nzuri Rais Dkt. Samia ameniteua kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya korosho Tanzania Sasa kwakuwa Mimi ni mkulima ni waahidi Walimu watakaohusika kwenye hizo ‘A’ kutakuwa na motisha na kwa kuanzia natenga shilingi laki tano.”
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Kimange, Ramadhani Kabelwa amewataka Wazazi kuhakikisha wanafika Wanafunzi wanarudi shule kuendelea na masomo mara baada muda wa likizo unapokwisha ili waweze kuendelea na masomo yao.
Aidha, amehimiza uimarishaji wa elimu ya msingi nchini ili Wanafunzi wakidhi mahitaji ya elimu ya Sekondari akisema, “wanakuja Wanafunzi kutoka shule za msingi lakini uwezo wao unakuwa bado ni mdogo kiasi kwamba Walimu wa Sekondari hulazimika kufanya kazi ya ziada ambayo ilitakiwa ifanywe na shule za msingi na kusababisha kuchelewa kwa Maendeleo ya wanafunzi hao katika ngazi ya Sekondari.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kimange, Wema Mbwana amesema Shule hiyo Ina eneo la kutosha la zaidi ya hela mia Moja ambazo zinaweza kutumika kwaajili ya shamba Hilo darasa la zao la korosho kwa Wanafunzi hao.