Kuanza kwa vikao vya Kamati ya pamoja ya Maridhiano ya Kisiasa kati ya Chama cha ACT -Wazalendo na Chama cha Mapinduzi – CCM, ni hatua muhimu ya kutia moyo na ya kuleta matumaini ya kuwepo na kuendelea mjadala wa masuala mbali mbali yanayohusu mustakabali mwema wa Zanzibar.

Hayo yamebainishwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman nyumbani kwake Chukwani , wakati alipokutana na Balozi mdogo wa Uingereza nchini Rick Shearn, aliyetaka kujua maendeleo ya Kamati hiyo ya pamoja iliyoundwa na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Amesema, tayari kwasasa Kamati hiyo imeanza vikao vyake kwa kujadili maeneo na agenda muhimu na makhususi na namna ya utaratibu bora utakaotumika katika kuyajadili masuala muhimu kwenye agenda hizo ili kuweza kufikia muafaka kwa malengo yaliyokusudiwa ya mustakabali wa Zanzibar na watu
wake.

Aidha, Othman pia amesema anaamini kwamba katika vikao hivyo vya awali maeneo yote muhimu yanayohitaji kufanyiwa mabadiliko na mageuzi makubwa yameainishwa kwa kuwasilishwa na kujadiliwa kwa pamoja katika kutafuta maslahi bora ya Zanzibar na watu wake.

Milango soko la Utalii yazidi kuifungukia Zanzibar
Adaiwa kumuuwa Mama yake kisha kumbaka