Chama cha Mapinduzi CCM Wilayani Kibaha mkoani Pwani kimewaonya wanachama waliokisaliti chama hicho wakati wa uchaguzi mkuu uliopita na sasa wamejitokeza kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho wasifanye hivyo kwani majina yao yanajulikana na yasipitishwe.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Idara ya Oganaizesheni ya Chama cha Mapinduzi CCM Makao Makuu Mjini Kibaha, Steven Kazidi, ambapo amesema kuwa watu hao walikisaliti chama bila haya wala aibu hivyo hakuna sababu ya kuwapa fursa ya kupitisha majina yao.

Amesema kuwa vikao husika vinavyopitisha majina ya wagombea visijaribu kuwabeba hata kidogo wanachama na viongozi waliobainika kukisaliti chama kwa kuwa walikuwa wakijionyesha hadharani sasa wanataka kugombea wasirudishwe.

“Tafadhali ,chonde chonde waliokisaliti chama na kujitokeza kugombea nafasi za chama na jumuiya kwa sasa wasipewe nafasi, natoa wito watu hawa wanajulikana wasipewe nafasi tena,”amesema Kazidi

Aidha amesema kuwa , wanachama waliochukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za chama waachane na habari ya safu na kuchafuana kwasasa wakati hatua zingine za uchujaji na kupitisha zikiendelea.

Hata hivyo, ameongeza kuwa kila mmoja agombee katika nafasi yake wasipangane safu kwa maslahi ya watu wanaotarajia kugombea ubunge kwenye uchaguzi mkuu 2020 ama uchaguzi wa serikali ya mitaa 2019 .

 

LIVE: Rais Magufuli awasili mkoani Singida kwa ziara ya kikazi
TRA yaidai Acacia kodi ya Trilioni 424, ni bajeti ya miaka 13