Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinazindua kampeni zake leo agost 29,2020, katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, ambapo wasanii zaidi ya 100 watashiriki kwenye jukwaa la uzinduzi huo kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2020

Tayari wananchi wameanza kufika uwanjani hapo kushuhudia uzinduzi huo ambao utaongozwa na mwenyekiti wa CCM taifa ambaye pia, ni mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

Dkt. John Magufuli, rais anayemaliza awamu yake ya kwanza amepewa ridhaa ya chama hicho kukiwakilisha kuwania katika ngazi ya urais kwa mara nyingine huku makamu wa rais akiwa Samia Suluhu Hassan.

Guillaume Soro aenguliwa kuwania urais
Ruksa wanafunzi wajawazito kuendelea na masomo- Zimbabwe