Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Chama Cha Rwandan Patriotic Front (RPF – Inkotanyi), Wellars Gasamagera, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.

Mara baada ya mazungumzo hayo Katibu Mkuu huyo wa Chama cha RPF – Inkotanyi pamoja na ujumbe wake watatembelea mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) pamoja na Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere (MNJLS), iliyopo Kwa Mfipa, Kibaha, mkoani Pwani.

Zifuatazo ni baadhi ya picha za kumbukumbu wakati na baada ya mazungumzo.

Tushirikiane kulinda vyanzo vya maji - Malisa
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Julai 2, 2023