Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeungana na vyama vingine vya siasa kuikosoa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kufuatia mapungufu yaliyojitokeza katika zoezi la kusaini maadili ya uchaguzi ya mwaka 2015.

Hali hiyo ijitokeza baada ya wawakilishi wa vyama mbalimbali vya siasa kukataa kusaini nyaraka zilizowasilishwa na tume hiyo baada ya kubainika kuwa karatasi 13 zilizopaswa kuwa sehemu ya nyaraka hizo hazikuwemo.

Akizungumza katika kikao hicho kilichowakutanisha viongozi wa vyama mbalimbali pamoja na viongozi wa tume hiyo, kabla ya kuvunjika, Makamu mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Philip Mangula alisema kilichotokea ni udhalilishaji.

“Tume mmetudhalilisha, inaonesha hamjajipanga,” alisema Mangula. “mmetuita kusaini maadili wakati hakuna kurasa 13 humu, hii lazima watu wawajibike,” aliongeza.

Awali, Katibu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi aliomba kutoa taarifa kabla ya kumsikiliza Makamu Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar, Hamid Mahamoud Hamid aliyetaka kusoma nyaraka za maadili ya uchaguzi ya mwaka huu.

Baada ya kupewa nafasi, Muabhi alieleza kuwa vyama vya siasa havina imani na tume kwa kuwa imekiuka makubalino ya kusambaza nyaraka hizo kwa vyama vya hivyo ili wazisome kabla ya kukutana kujadili.
Mwisho, Jaji Hamid aliwaomba radhi wajumbe na kuahidi kuyafanyia kazi mapungufu hayo kabla ya kuitisha kikao kingine na vyama vya siasa.

Baada Ya Kugonga Mbili, Busungu Atoa Ya Moyoni
Ester Bulaya Ameikwepa Ngumi Ya ‘Tyson’ CCM