Chama cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga Mjini mkoani Shinyanga kimefanya Kongamano ikiwa ni uzinduzi wa wiki ya Maadhimisho ya miaka 40 tangu kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM tarehe 05.02.1977.
…………………………………………………………………..
…………………………………………………………………..
Kongamano hilo limefanyika Ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa wilaya za mkoa huo, makada wa CCM na vyama vya upinzani na watu mbalimbali wakiwemo wanafunzi wa Shule za sekondari.
Mada mbalimbali zimetolewa wakati wa kongamano hilo ikiwemo historia ya CCM na mafanikio ya chama hicho tangu kuanzishwa kwake mwaka 1977.
Katika kuadhimisha wiki ya maadhimisho ya miaka 40 ya CCM,Chama cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga kitashiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo katika ngazi ya matawi ikiwemo,kupanda miti,kusalimia wagonjwa,watoto yatima,walemavu,kutembelea shule,michezo na kufanya mikutano ya ndani badala ya mikutano ya hadhara.
Vyama asili vilivyozaa CCM ni Tanganyika African National Union (TANU) cha Tanganyika na Afro Shiraz Party (ASP) cha Zanzibar vyote vikiwa ni vyama vya ukombozi.
Aidha, Kauli mbiu ya maadhimisho ya miaka 40 ya CCM ni “CCM Mpya,Tanzania Mpya”