Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi – CCM, iliyokutana hii leo Oktoba 22, 2023 mjini Dodoma, katika kikao chake maalum, chini ya
Mwenyekiti wa CCM, Samia Suluhu Hassan, imeridhia kwa kauli moja na kuielekeza Serikali
kuendelea na hatua ya utiaji saini mikataba ya uendelezaji na uwekezaji wa Bandari.

Aidha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, imefanya mabadiliko madogo ya Sekreterieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kwa kumteua
Paul Makonda kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi, akichukua nafasi ya Sophia Mjema ambaye ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais Masuala ya Wanawake, Watoto na Makundi Maalum.

Halmashauri Kuu ya CCM Taifa pia imemteua Ndugu Rabia Abdallah Hamid kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Siasa na
Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), akichukua nafasi ya Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Afrika Mashariki.

Aidha katika kikao hicho, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imezipongeza Serikali zake zote mbili, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
chini ya Rais Dokta Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, chini ya Rais Hussen Ali Mwinyi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, kwa kazi kubwa na nzuri ya
kuendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020-2025.

Kumbukizi ya Nyerere yamalizia ujenzi Kambarage
TAMWA-ZNZ yavunja ukimya ukosefu wa maadili kwa Vijana