Scolastica Msewa, Kibaha – Pwani.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi – CCM, Mkoa wa Pwani, Mwinshehe Mlao amewataka Wazazi wa wazawa wa Mkoa wa Pwani kusomesha watoto wao, ili waweze kunufaika na fursa za uwekezaji mkubwa unaoendelea Mkoani Pwani.

Akihutubia Wananchi wakati Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Pwani ilipofika kukagua utekelezaji wa Ilani katika Shule mpya ya Sekondari ya Kata ya Mkuza iliyopewa jina la Msimbo huko Msangani Kibaha amesema Serikali tayari imetimiza wajibu wake wa kujenga Miundo Mbinu ya elimu na Wazazi kuwapeleka shule na kuwasimamia.

Amesema, kazi kuu ya mtoto ni kumsomesha na si kumfisadi kwa kumpatia kazi ambazo zitamwingiza kwenye vitendo vitakavyomkatiza masomo yake, huku akitaja baadhi ya shughuli ambazo Wazazi wa mkoa wa Pwani huwafisadi watoto wao kuwa ni pamoja na uuzaji wa biashara za mikononi Barabarani na upigaji debe wa mabasi ya abiria badala ya kwenda shule.

Awali, Meneja msaidizi wa mradi wa Bandari Kavu Kwala Eng. Gabriel Mwangosi amesema lengo la kuanzishwa kwa bandari hiyo ni kupunguza asilimia 30 ya msongamano wa makontena katika Bandari ya Dar -es
– Salaam na kutengeneza Mazingira mazuri ya huduma za Bandari kwa wateja wao hususani mataifa mbalimbali yanayohudumiwa na Bandari.

Amesema, “yale mataifa yanayohudumiwa na Bandari ya DSM kama nchi yamepewa maeneo yao katika eneo hilo la Bandari Kavu ya Kwala ambazo ni nchi za Rwanda, Zambia, Congo lengo likiwa ni kushusha makontena 3000 kwa Siku sawa na Makontena laki 8 kwa mwezi.”

Kuhusu mradi wa Kongani ya Viwanda, Mwenyekiti wa SINO TAN,Jauson Huang amesema mradi huo ulianza mwezi may 2022 huku ukiwa na awamu tatu hadi kukamilika, ingawa awamu ya kwanza inatarajia kumalizika mwezi Desemba 2023.

Kamati hiyo, ikiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kibaha ilikagua Maendeleo na huduma zinazotolewa katika Hospitali ya Wilaya hiyo ili iweze kutoa huduma kwa ufanisi inahitaji kuwa na korido zinazounganisha jengo Moja kwenda jingine yenye urefu wa MITA 915 kufanya zaidi ya milioni 523 zinahitajika ili kukamilisha mpango huo.

Tumieni fursa za uwekezaji, toeni ushirikiano – Majaliwa

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Kibaha Dr. Christopher Ngendello amesema hadi kufikia October, 2023 jumla ya wagonjwa 5272 wamehudumiwa katika Hospitali hiyo na kudai kuwa tangu kuanza kwa huduma ya X Ray na Ultra Sound Hospitalini hapo kumepunguza Idadi ya Rufaa zinazoenda Hospitali ya Mkoa ya Tumbi na kuweza kutibiwa Hospitalini hapo ambapo wagonjwa waliopatiwa huduma ni 759, kati Yao X ray ni 589 na Ultra sound 170.

Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Pwani ikiwa katika Halmashauri ya Mji Kibaha pia ilitembelea na kukagua Utekelezaji wa Ilani Katika miradi ya Shule mpya ya Sekondari ya Shimbo Mkuza, Ujenzi wa barabara kwa kiwango Cha lami yenye urefu wa Km. 0.7 iliyopo picha ya ndege – Bokotimiza yenye thamani ya Shilingi bilioni 1 kupitia tozo za mafuta, na Soko la Kisasa lililopo katika Kata ya Tangini ambalo limekamilika kwa asilimia 99.5 na kugharimu jumla ya shilingi 8 Bilioni.

Sikio la kufa: Wengine wadakwa wakisafirisha Mifugo kwa magendo
Zanzibari yafungua fursa za kiuchumi kwa Waromania