Chama cha Mapinduzi CCM kimelaani tukio lililotokea hii leo mjini Dodoma la kupigwa risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu.

Aidha, katika taarifa iliyotolewa na Katibu wa NEC- Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole imesema kuwa chama kimepokea kwa mshtuko shambulio hilo na kinalaani kutokea kwa tukio hilo.

“Chanma cha Mapinduzi (CCM) kinalaani tukio hilo la kikatili na lisilo na utu na tunalitaka jeshi la polisi kuwatafuta na kufanya uchunguzi wa tukio hili ili hatua kali zichukuliwe dhidi ya waliotekeleza tukio hilo,”amesema Polepole.

Hata hivyo, taarifa hiyo imeongeza kuwa Uongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM unamwobea mwanasiasa huyo apone haraka ili aendelee na majukumu yake ya chama na kibunge.

 

Hii ni laana kwa viongozi kula mali za umma- Ndugai
Kikwete, Zitto wanena makubwa kuhusu Lissu