Saa chache baada ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif kuweka hadharani msimamo wake na chama chake kufuatia mazungumzo ya kutafuta ufumbuzi wa mkwamo wa kisiasa visiwani Zanzibar akidai kuwa hawakubaliani na uamuzi wa kurudia uchaguzi, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewajibu.

Akizungumza jana katika viwanja vya Maisara visiwani Zanzibar ambapo viongozi wa ngazi za juu wa CCM walikuwa wamekusanyika kwa  matembezi ya kuunga mkono mapinduzi ya Zanzibar, Makamu wa pili wa rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi alisisitiza kuwa uchaguzi huo lazima urudiwe na kinachosubiriwa ni tangazo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi (ZEC).

Alisisitiza kuwa hata kama vyama vyote vya upinzani havitashiriki uchaguzi huo, CCM itashiriki yenyewe. Kadhalika, aliwatahadharisha CUF kuhusu kauli yao ya kutumia nguvu ya umma na kueleza kuwa watayaona matunda yake.

“Uchaguzi wa marudio upo pale pale, tunajua uchaguzi ulifutwa kihalali, mjitayarishe kwa uchaguzi wa marudio. CUF wamesema watatumia nguvu ya umma, tunawakaribisha na wataona matokeo yake,” alisema Balozi Iddi.

Ronaldo akiri kuutamani mguu wa Messi
'Zanzibar Majipu Yapo'