Wakati ambapo leo Chadema wanatarajia kuzindua kwa kishindo kampeni katika viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam, CCM wamemuwekea mtego mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa kwa kuyahesabu maneno yake kwa jinsi atakavyozungumzia sakata la Richmond.

Chama hicho kimemtahadharisha Lowassa kuwa endapo leo atakanusha kuhusika na sakata Richmond lililomsababisha kujiuzulu nafasi yake ya uwaziri mkuu mwaka 2008, chama hicho kitatoa taarifa za ziada ambazo hazikutolewa bungeni kuhusu sakata hilo.

CCM imeenda mbali zaidi na kueleza kuwa bado kinayo nafasi ya kumshitaki Lowassa kwa ‘kesi ya magendo’ kwa kuwa kesi ya jinai haifi.

“Kwa sasa ninasubiri kesho (leo) wakati wa uzinduzi wa Ukawa kama litagusiwa, nitaweka wazi mambo yote ambayo hayakuongelewa bungeni kipindi kile,” alisema Harison Mwakyembe aliyekuwa mwenyekiti wa kamati maalum iliyochunguza sakata hilo.

Mwakyembe ambaye ni mmoja kati timu ya watu 32 iliyoteuliwa na CCM kuongoza kampeni za kumnadi mgombea urais wa chama hicho, Dk. John Magufuli aliyasema hayo jana jijini Mbeya wakati akihutubia katika mkutano wa kampeni.

Aliwataka wananchi hao kuhakikisha wanamchagua Dk. Magufuli kwa kuwa anauchukia ufisadi na amepanga kuanzisha mahakama maalum ya kushughulikia kesi za ufisadi endapo atachanguliwa kuwa rais wa Tanzania.

Lowassa Aipiku Ahadi Ya Magufuli
Lowassa: Yatakwisha Baada Ya Siku 60