Chama cha Mapinduzi (CCM) kimejibu kwa mara nyingine kauli ya Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad ya kuwataka wananchi kukaa tayari kwa mabadiliko ya uongozi visiwani Zanzibar.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Abdallah Juma amewataka wananchi kupuuza kauli hizo na kuendelea na shughuli zao za kila siku kwani hawajawahi kufanya mazungumzo yoyote na Maalim Seif.

“Hatujawahi kukaa na mahasimu wetu hao hata siku moja kujadili suala la hali ya kisiasa Zanzibar,” Dkt. Juma anakaririwa. “Wao wana kazi zetu za kisiasa na sisi tuna kazi zetu ambazo tunaendelea kuzifanya ili kujiweka tayari kwa uchaguzi wa mwaka 2020,” aliongeza.

Dkt Juma ametoa kauli hiyo kujibu kauli ya Maalim Seif aliyoitoa hivi karibuni katika sherehe za mahafali ya Jumuiya ya Vijana wa CUF (Juvcuf) ambapo aliwataka kuwa tayari kwa mabadiliko ya uongozi hivi karibuni.

Maalim Seif alisusia uchaguzi wa marudio uliofanyika baada ya kufutwa kwa uchaguzi wa Oktoba 25, 2015.

Mwakyembe apiga marufuku tuzo za muziki na mashindano ya Miss Tanzania
Wanaume suruali kukiona kwa wake zao.