Saa chache baada ya kusambaa picha zinazomuonesha Rais John Magufuli akisalimiana na ‘kuteta’ na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, wasomi na baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameisifia hatua hiyo.

Rais Magufuli na Lowassa ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema walikutana katika sherehe za Jubilee ya dhahabu ya ndoa ya Rais wa Awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na mkewe mama Anna Mkapa katika kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro lililoko jijini Dar es Salaam.

Lowassa na Magufuli

Kadhali, Lowassa alisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na wawili hao walionekana kufurahia jambo pamoja.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulahman Kinana

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana

Akizungumzia tukio hilo, msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka alimsifu Lowassa akieleza kuwa amekuwa akimfahamu kuwa ni mtu muungwana na asingeweza kukataa kusalimiana na Rais Magufuli kutokana na tofauti zao za kisiasa na mvutano uliopo.

“Namfahamu Lowassa ni muungwana, hawezi kuacha kusalimiana na kupeana mkono na Rais. Wamekutana viongozi, Rais na waziri mkuu mstaafu hawawezi kuacha kusalimaina,” Ole Sendeka anakaririwa.

Sendeka aliongeza kuwa hizo ni dalili nzuri na kwamba anaamini hakutakuwa na vurugu Septemba 1, siku ambayo Chadema walitangaza kufanya operesheni UKUTA.

Katika hatua nyinginge, Mwanasheria wa Chadema ambaye pia ni mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu alipongeza hatua hiyo na kueleza kuwa hilo ni suala jema linalotoa picha ya dalili njema.

“Chini ya salamu za Obama na Raul (Rais wa Cuba), kulikuwa na mazungumzo yaliyosababisha kurudishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya Marekani na Cuba,” Lissu amesema kwenye tamko lake mitandaoni ambalo amelithibitisha.

Aliongeza kuwa kama viongozi hao waliteta pia kuhusu UKUTA itafahamika baadaea huku akiwataka wanachama wa Chadema kuendelea na maandalizi ya Operesheni hiyo wakisubiri.

 

Polisi yasema Lema Kugoma Kula ‘ni Kosa la jinai’, Mwanasheria wake atangaza hatua
Baraza Kuu CUF 'lawatumbua' Profesa Lipumba na Sakaya