Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimekubali kushiriki katika mdahalo kufuatia ombi la vyama vya upinzani vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) huku kikitoa masharti kuhusu washiriki wa mdahalo huo.

Akiongea kwa niaba ya chama hicho, Mbunge wa Bumbuli ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya kampeni ya CCM, January Makamba amesema kuwa chama chake kiko tayari kufanya mdahalo ulioombwa na mwenyekiti mwenza wa Ukawa, January Makamba endapo washiriki wa mdahalo huo watakuwa wagombea urais wenyewe na sio wawakilishi wao.

“Wenzetu wa Ukawa wamesema mdahalo uwe kati ya wawakilishi wa chama, itakuwa mara ya kwanza duniani kwenye uchaguzi wagombea wanawakilishwa kwenye mdahalo na watu wengine,” Makamba alisema.

“Lakini upande wa pili ni kwamba jana wenzetu wamesema wanaomba mdahalo, ukweli ni kwamba mualiko wa mdahalo ulitumwa kwa vyama vyote wiki tatu zilizopita na sisi tuliupokea na tulikubali kushiriki,” aliongeza.

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, ambaye ni mwenyekiti mwenza wa Ukawa, James Mbatia aliwataka CCM kushiriki mdahalo wa pamoja na Ukawa kwa kuwachagua wenyeviti wa vyama hivyo kuzitetea ilani ya vyama vyao.

“Tunawataka CCM waje kufanya mdahalo kwa hoja, wenyeviti wa vyama wawekwe kwenye mdahalo ili ukawa tupambane na CCM kwa hoja na watanzania wajue pumba na mchele,” Mbatia alikaririwa.

Lowassa Aiteka Chato Kwa Magufuli, Picha Sita
CCM Yataja Matokeo Ya Utafiti Wa Ushindi Waliopata, Ukawa Nao Wataja Ushindi Wao