Chama cha Mapinduzi kimeshinda uchaguzi wa Ubunge katika jimbo la Ulanga lililoachwa wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo aliyefariki wakati kampeni za uchaguzi huo zikiendelea, Celina Kombani.

Msimamizi wa uchaguzi huo jana (Novemba 22) alimtangaza mgombea kupitia CCM, Goodluck Mlinga kuwa mshindi baada ya kupata kura 25,902 sawa na asilimia 69.78 dhidi ya mshindani wake mkuu kupitia Chadema, Pancras Michael aliyepata kura 10,592 sawa na asilimia 28.53.

Ushindi mkubwa wa kada huyo wa CCM unampa nafasi ya kurithi kijiti cha mtangulizi wake marehemu Celina Kombani ambaye alisifika kwa utendaji wake wa kazi na jinsi alivyowatumikia wananchi wa jimbo hilo.

 

 

Kufutwa Sherehe Za Uhuru 'Disemba 9' Mwisho Uko Hapa...
Magufuli Afuta Sherehe Za Uhuru za Disemba 9