Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimetangaza neema kwa wafanyakazi wadogo endapo watakichagua tena kuongoza serikali ya awamu ya tano. Kimeeleza kuwa kitafuta ushuru kwa wafanyabiashara wote wadogo.

Hayo yamesemwa na mgombea mwenza wa urais kupitia chama hicho, Bi. Samia Suluhu alipokuwa akiwahutubia wananchi wa mkoa wa Shinyanga hivi karibuni katika moja kati ya mikutano yake ya kampeni.

Mkutano Samia

“Tutakachofanya ni kurasimisha sekta ya wafanyabiashara wadogowadogo. Kuwafanya wawe rasmi na wajulikane kisheria. Na ni kwa ajili hiyo, kodi zitakazotozwa ni zile kodi za kisheria na sio zile kodi na ushuru wa hapa na pale kama unavyotozwa sasa hivi,” alisema.

Bi. Samia aliongeza kuwa serikali watakayoiunda itatengeneza fursa zaidi kwa wafanyakazi wadogowadogo ili waweze kujiunga na huduma ya mifuko ya kijamii pamoja na taasisi za kifedha ili waweze kukopesheka.

Yanga Wamalizana Na Mwambusi
Picha: Lowassa Alivyoitikisa Musoma, Mapokezi Yavunja Rekodi Kwa 'Mbwembwe'