Chama cha mapinduzi mkoani Kagera kimekiri kutokea kwa changamoto mbalimbali wakati wa mchakato wa kuteua na kupiga kura za maoni na kuwataka wanachama kuendelea kuwa na imaani na chama chao.

Akiongea na waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu ya chama hicho mkoani Kagera MNEC wa mkoa huo Wilbroad Mutabuzi amesema kuwa zimetokea changamoto nyingi katika uchaguzi wa kura za maoni zilizopelekea kurudiwa kwa uchaguzi katika baadhi ya maeneo katika wilaya za Muleba na Bukoba.

Mutabuzi amesema kuwa kanuni nyingi zilivunjwa wakati wa uteuzi wa wagombea pamoja na mchakato mzima nakubainisha baadhi ya dosari zilizojitokeza chama kimejipanga kuzifanyia kazi.

“Ni kweli changamoto zimejitokeza katika uchaguzi na uteuzi wa wagombea katika nafasi za wenyeviti wa vitongoji na vijiji na Serikali za Mitàa, sasa hivi changamoto hizo tumezifanyia kazi na tayari katika baadhi ya maeneo uchaguzi umerudiwa na pengine utarudiwa.” Amesema Mutabuzi.

Aidha amesema kuwa baadhi ya changamoto zilizojitokeza ni pamoja na wagombea waliohamia CCM kutoka vyama vingine kuteuliwa na wale waliokuwa kwenye chama hicho kuachwa, kuchelewa kupigwa kura katika baàdhi ya maeneo na rufaa za baadhi ya wagombea kutopelekwa kwa wakati katika ofisi za chama wilaya ili waliokata rufaa hizo kupata haki zao.

Mutabuzi amewataka wananchi waliojiandikisha kujitokeza kwa wingi wakati utakapowadia wa kupiga kura na kuhakikisha wakati wa kampeni wanafanya kwa utulivu na kulinda amani ya nchi yetu ili kuweza kuzuia hali ya uvunjifu wa amani

Video: Membe avuruga serikali, CCM, JPM amedhamiria kweli
Asimulia penzi la usiku mmoja lilivyomponza, 'wasichana bebeni mipira kwenye mikoba yenu'