Spika wa Bunge la 11, Job Ndugai amesema kuwa bunge hilo linaongoza kwa kuwa na wasomi wengi kulinganisha na mabunge yaliyopita kutokana kuwa na idadi kubwa ya wasomi ambapo 29 ni wenye shahada za Uzamivu (PHD)  na 159 wakiwa na Shahada ya kwanza.

Ndugai ametoa takwimu hizo na kusema kuwa katika shahada za Uzamivu (PHD), 29 kati ya hizo 27 zinamilikiwa na wabunge wa Chama Cha Mapinfuzi (CCM), 1 ikimilikiwa na mbunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), na 1 kutoka Chama cha Wananchi (CUF).

Upande wa Shahada ya Kwanza ambazo jumla zipo 159, shahada 14 zinamilikiwa na Wabunge wa CUF, 31 kutoka kwa wabunge wa Chadema na 114 kutoka kwa wabunge wa CCM.

Aidha, amesema kuwa Mbunge mwenye umri mdogo kuliko wote ni Halima Abdalah Bulembo ambaye ni Mbunge wa Viti maalumu (CCM) kutoka Bukoba ambaye alianza ubunge akiwa na umri wa miaka 24 na sasa ni mwenye umri wa miaka 27 aliyezaliwa April 1, 1991 na kuteuliwa rasmi kuwa mbunge wa viti maalumu katika bunge la 11 2015.

Hata hivyo Ndugai amesema katika Bunge la 11 Mbunge mkubwa kuliko wote ana umri wa miaka 75 ambaye ni Nimrod Mkono huyu ni Mbunge mteule kutoka Butiama mwenye umri wa miaka 75, ambaye wakati wa uteuzi wake alikuwa na miaka 72 mnamo 2015.

Ameongezea kuwa wabunge wenye umri wa miaka 40 na zaidi ni 80% ya wabunge wote hivyo na kusema Bunge la 11 si bunge la vijana.

 

Warembo 8 kutoka Afrika wanaoelekea 'Miss World 2018'
Watabiri wa hali ya hewa waonya kuhusu kimbunga Florence