Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimepitisha marekebisho yaliyofanyika kwenyea Katiba ya chama ikiwemo idadi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu (NEC), ambazo zitakuwa Tanzania Bara 20 na Visiwani Zanzibar 20 badala ya 15 kwa kila upande, kama ilivyokuwa hapo awali.
Kupitia wajumbe hao wa Mkutano Mkuu unaofanyika hii leo Desemba 7, 2022 jijini Dodoma, pia nafasi za uteuzi kwa wajumbe wa NEC zinaongezeka kutoka sita hadi 10, huku nafasi ya ukatibu wa siasa na uenezi wa mikoa kuwa ya ajira badala ya kuteuliwa na kupitishwa kwa kukubaliana na mabadiliko hayo baada ya Mwenyekiti wa CCM kutoa hoja.
Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameeleza sababu mbalimbali za mabadiliko hayo ya katiba hasa nafasi ya uenezi kuwa ya kuajiriwa akisema, “Inawezekana kuna sababu nyingi labda uwezo au nyingine, tumeona ili chama kisimewe vizuri kuanzia ngazi ya mkoa nafasi ya uenezi iwe ya ajira.
Aidha, Mwenyekiti huyo amefafanua kuwa, “Hatua hii itafanya awajibike vizuri kukisemea chama, kwa sababu ni nafasi ya ajira itakuwa ina vipimo kwamba unafanya vizuri utaendelea au unafanya vibaya mkataba utasitishwa ili awekwe mwingine atakayekuwa na sifa ya kukisemea chama.”