Uongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Njombe wakiongozwa na mwenyekiti wao mkoani humo, Jasel Mwamwala, wamesema kuwa wamesikitishwa na vitendo vya kuwateka na kuwaua watoto wadogo vinavyoendelea mkoani humo vinavyohusishwa na Imani za kishirikina.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa CCM mkoani humo, Jesel Mwamwala alipokuwa akizungumza mbele ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni, ambapo amewaomba wananchi wa Njombe waendelee kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama ili kuweza kuwabaini wahusika wa matukio hayo.
“Chama cha Mapinduzi hakita muacha salama mtu yeyote anayezusha taarifa zisizo za kweli, Tanzania ni moja ya nchi za kuigwa kwakuwa bado ni kisima cha amani tangu miaka mingi iliyopita hivyo hawatakuwa salama wanaoendelea kuichafua serikali yetu ya Tanzania kupitia vitendo hivi vya kikatili, wananchi toeni taarifa zenye uhakika ili sheria ichukue mkondo wake,”amesema Mwamwala
Naye mwenyekiti wa CCM wilaya ya Njombe, Edward Mgaya amewaasa wananchi wa Njombe kutoa taarifa za ukweli kuhusu matukio ya mauaji yanayoendelea kwasasa ili kuweza kurahisisha kuwabaini wahusika na kuutokomeza mtandao huo.
-
Chadema wamgomea Askofu Kakobe, ‘katubu mwenyewe’
-
Kada wa CCM Njombe akabidhi Miche 500 ya Parachichi
-
Ofisi ya Mbowe bado utata mtupu, Katibu, DC wajibizana
kwa upande wake Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni ameliagiza Jeshi la Polisi Mkoani humo kuongeza jitihada za kukabiliana na wahalifu hao ikiwemo kuweka vizuizi na kukagua magari yote yanayoingia na kutoka katika Mkoa wa Njombe.