Ushindani mkubwa unaoshuhudiwa katika kampeni za uchaguzi mkuu mwaka huu umepelekea kila upande kuhakikisha inatoa sifa zote za mgombea wao kadri inavyowezekana kwa nia ya kushawishi, sifa ambazo wakati mwingine huwaacha baadhi mdomo wazi.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ambaye amekuwa akimwagia sifa za kipekee mgombea urais kupitia chama hicho Dk John Magufuli, jana akiwa Mirirani, Manyara, alisema kuwa mgombea huyo anamiliki simu moja tu tofauti na wanasiasa wengine na kudai kuwa inasaidia kumpata mara moja unapomhitaji.

“Huyu ndiye mbombea tunayemtaka, hana makuu, ukitaka kumpata unampigia simu mara moja, siyo wengine wanazo nne na hujui utampataje,” Kinana ananukuliwa na gazeti la Mwananchi.

Katibu Mkuu huyo alikuwa katika mji mdogo wa Mirirani, Manyara kwa ajili ya kumsimika Daniel Ole Materi kuwa kamanda wa UVCCM wilaya ya Simanjiro.

Balotelli Achangia Ushindi Wa AC Milan
CCM Na Chadema Wakwepa Mdahalo Wa Urais, Waishia Tambo