Chama Cha Mapinduzi – CCM, Kata ya Mkange Bagamoyo mkoani Pwani, kimeagiza kupelekwa kwa haraka Wahudumu wa Afya wakike katika Zahanati ya kijiji cha Gongo na Zahanati ya kijiji cha Matipwil, ambako Wananchi wanapata shida kwa kukosa huduma toka kwa watabibu wa jinsia hiyo.

Akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Gongo wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa ya Kata ya Mkange, Mwenyekiti wa CCM wa Kata hiyo, Abdallah Dimauya amesema katika vijiji vya Gongo na Matipwili hakuna kabisa Wahudumu wa afya mbali na kukosekana kwa Wahudumu wa jinsia ya kike.

Amesema, “hakuna Nesi kabisa hili jambo linatakiwa lifanyiwe kazi haraka kwani Kuna Madaktari wakiume wakiwa anaumwa au wakisafiri huduma za afya hazipatikani na ukizingatia jinsia ya kike masuala ya uzazi hakuna anayeweza kuwahudumia kulingana na jinsia zao.”

Kuhusu suala la elimu katika eneo hilo, Dimauya amesema kuna boma la Shule ya msingi lililojengwa tangu mwaka 2019 hadi leo na halijapata kuendelezwa mbali ya Wananchi kujitolea kwa asilimia kubwa katika ujenzi huo na hivyo kuwasisitiza Viongozi husika kushughulikia suala hilo.

Ushirikiano silaha kuu ya kuzuia uhalifu - Polisi
Mchungaji mbaroni kwa ulaghai wa uchawi Kanisani