Chama cha Mapinduzi CCM kimeibuka na ushindi katika kata 42 kati ya 43 zilizofanya uchaguzi mdogo wa udiwani jumapili ya Novemba 26 kwenye mikoa 19 nchini.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam akitoa tathmini ya uchaguzi huo.

Amesema kuwa Chama chake kimeibuka na ushindi huo katika kata hizo ikiwa ni matokeo ya kazi nzuri inayofanywa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya CCM.

Aidha, Polepole ameitaja kata ambayo chama chake kimekosa ushindi kuwa ni Ibigi iliyopo wilayani Rungwe mkoani Mbeya ambayo imechukuliwa na mgombea wa CHADEMA.

Hata hivyo, Polepole amezitaka mamlaka kushughulikia haraka baadhi ya dosari zilizojitokeza kwenye baadhi ya maeneo ambayo chama hicho kimeripoti kutoridhishwa na mwenendo wa mchakato wa uchaguzi ikiwemo vitendo vya vurugu.

 

 

Sakaya: Bora kustaafu siasa kuliko kuhama chama
Serikali kugawa Kondomu bure