Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha kinadaiwa kuwafukuza uanachama baadhi ya vigogo wake akiwamo Mwenyekiti wa chama hicho Wilaya ya Arusha, Wilfred Soileli.
Wanachama hao wanatuhumiwa kukisaliti chama hicho kabla na baada ya uchaguzi mkuu wakidaiwa kuwa wafuasi watiifu kwa Waziri Mkuu wa zamani aliyejiuzulu, Edward Lowassa.
Aidha, wengine waliotimuliwa ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa kutoka jimbo la Arumeru Magharibi Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC ) na mfanyabiashara maarufu wa madini ya vito, Mathias Manga na Julius Mungure wa Jimbo la Arumeru Mashariki.
Wakati vigogo hao mkoani Arusha ikielezwa kuvuliwa uanachama wiki iliyopita, Kamati ndogo ya Maadili ya CCM iliyokutana Dodoma iliwahoji wanachama wake ambao wanadaiwa kukisaliti chama hicho.
Aihda waliohojiwa mjini Dodoma ni Prof. Juma Kapuya, Nazir Karamagi na Ally Sumaye ambao wote wanadaiwa kukisaliti chama wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Hata hivyo, baadhi ya wajumbe wa kikao hicho wamesema kuwa Soileli na Manga walituhumiwa kushirikiana kutoa siri na mikakati ya chama na kuipeleka kwa viongozi wa Ukawa hasa Lowassa ambaye alikuwa mgombea wa nafasi ya Rais.

Bunge la 11 laweka histoiria nyingine
Vigogo watema 'cheche' kuhusu dawa za kulevya