Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama nchini Venance Mabeyo amewathibitishia wananchi wa Ukerewe mkoani Mwanza na Tanzania kwa ujumla kuwa kivuko kilichozama wiki chache zilizopita cha MV Nyerere kimenyanyuka kwa asilimia 85% na kitatolewa majini ili kuanza kwa matengenezo ya kivuko hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari mkuu huyo wa majeshi alisema kuwa serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imefanikisha zoezi la kukitoa kivuko hicho kilichokuwa kimezama na kisha kukiinua tayari kwa kupelekwa nchi kazi.
Aliongeza kuwa jeshi la wananchi liliwahakikishia wananchi kuwa ni lazima kivuko hicho kinyanyuliwe kwa uangalifu wa hali juu ili kama kuna miili ya watanzania wengine ambao walikandamizwa na kivuko hicho miili yao iweze kuonekana kwa urahisi zaidi na kuchukuliwa kwa ajili ya kuhifadhiwa.
“Serikali ya Tanzania inamalengo makubwa ya kuwasaidia wananchi wake katika kila jambo, liwe zuri au baya kwa lengo la kuwajali”Amesema Mabeyo.
Aidha mkuu huyo wa majeshi aliwapongeza wale wote walioonyesha ushirikiano mkubwa katika kufanikisha zoezi hilo, pia amewapongeza msalaba mwekundu, madokta na manesi waliojitolea katika kuhakikisha wanawahifadhi ndugu zetu walipoteza maisha katika ajali hiyo.
Aliongeza kuwa jeshi la wananchi linaendelea na uokoaji wa watu waliobaki majini kama bado wapo ingawa wanajeshi wazamiaji bado wanaendelea na usakaji wa miili ya watu na vifaa mbalimbali.
-
Breaking News: Rais Magufuli akizindua Flyover muda huu
-
Video: Mgaya awapiga dongo wapinzani, ataka washindane kwa hoja
-
JPM ataja sababu ya kuita Mfugale flyover
Pia mkuu huyo wa majeshi amewapongeza waandishi wa habari kupitia vyombo mbalimbali kwa jinsi walivyojitoa katika kuhabarisha umma juu ya kile kilichotokea katika kisiwa cha ukara wilayani ukerewe kwa wananchi wote walioko mbali na mkoa huo na hasa kwa kusema ukweli.