Tanzania Bara inatarajiwa kucheza na timu za Ethiopia, Zambia na Somalia katika mashindano ya Chalenji maarufu kama CECAFA Challenge Cup yatakayofanyika nchini Ethiopia baadae mwezi huu.

Tanzania Bara itacheza na timu hizo kufuatia kupangwa kundi moja na timu hizo ambapo mashindano yenyewe huenda yakafanyika kati ya Novemba 21 na Desemba 6 mwaka huu.

Kwa mujibu wa tovuti ya Kawowo Sports ya nchini Uganda, makundi hayo yametokana na droo iliyochezeshwa leo huko mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.

Kenya ndiyo bingwa mtetezi baada ya kushinda taji hilo mwaka 2013 kwenye fainali zilizopigwa mjini Nairobi.

Ikumbukwe kwamba mashindano hayo hayakuweza kufanyika mwaka jana baada ya nchi zilizotarajiwa kuwa mwenyeji kupigiana danadana ikiwemo Ethiopia.

MAKUNDI YA CECAFA 2015

Group A: Ethiopia, Zambia, Tanzania, Somalia

Group B: Kenya, Uganda, Burundi, Djibouti

Group C: Sudan, Rwanda, South Sudan, Zanzibar.

Urusi Hatarini Kufungiwa Na IAAF
Chelsea Yaangalia Uwezekano Kwa Diego Pablo Simeone