Rasmi Yanga SC imeingia mkataba wa miaka miwili na kocha wao mpya raia wa Burundi Cedric Kaze, ambaye ametua nchini usiku wa kuamkia leo Oktoba 16, 2020 Kocha Kaze anachukua nafasi ya Zlatko Krmpotic, ambaye alitimuliwa hivi karibuni baada ya kuifundisha timu kwa siku 37 tu.

Baada ya kusaini, Kaze, ambaye ni Kocha wa zamani wa timu za vijana za Burundi za miaka 17, 20 na 23 na ile ya wakubwa; amesema hana maneno lakini vitendo vitarajiwe ndani ya Uwanja.

“Najivunia kuwa kocha mpya wa Yanga yenye historia, timu yenye mashabiki wa aina yake na miongoni mwa timu bora za Afrika – Mimi nataka timu yangu ichezee mpira, imiliki mpira na tucheze eneo la mbali na lango langu ili hata tukipoteza mpira isiwe rahisi mpinzani wetu kufika kwetu kabla hatujajipanga”.

“Sichezeshi wachezaji 11 bora uwanjani nachezesha timu bora uwanjani Sichezeshi jina wala staa… nachezesha timu ambayo italeta mafanikio na usishangae mchezaji mkubwa akawa anakaa benchi. Tunaangalia timu zaidi,”

“Hatutaki mpira wa ”show’ tunataka mpira wa kwenda mbele hapa mnaita sijui kucheza na jukwaa mimi sitataka hiyo, zaidi nataka timu ishinde sio mchezaji kuonyesha sifa binafsi – Kwasasa niseme tu nafurahia wachezaji waliopo tunawachezaji bora na mimi nitapenda nifanye nao kazi kwa muda mrefu”.

Zlatko kuishtaki Yanga FIFA
Wafuasi 132 wa Bobi Wine wakamatwa