Nguli wa muziki kutoka Marekani, na mkongwe Celine Dion ametangaza rasmi ujio wa albamu yake mpya ‘Courage’ itakayoingia sokoni November 15 mwaka huu na itakuwa albamu yake ya kwanza bila ushiriki wa marehemu mume wake Rene huku akimtaka Drake kuacha kuchora mchoro  wa sura yake katika mwili wake ‘Tatoo’ kwani hauna manufaa yoyote

”Usifanye hivyo” aliongea kwa msisitizo unaweza kuandika barua pepe za upendo, unaweza kunitumia autograph kwaajili ya watoto wangu, unaweza kunitembelea amesema Celine

Katika hatua nyingine msanii huyo ameeleza kuwa sura yake inabadilika jinsi muda unavyokwenda wala si kitu kilichokuwa kinatengeneza hela kwenye fani yake anaamini tatoo yake kwenye mwili wa Drake haitakuwa na mwisho mzuri kumfanya rappa huyo awe na muonekano wa jabu atakapozeeka.

Rapa huyo anaesifika kwa mahaba yake ya ajabu kila anapomtunuku mtu huamua kuichora sura ya muhusika kwa mfumo wa tattoo.

Akizungumza kuhusu albamu yake amesema kuwa ina nyimbo nyingi zinazoeleza maisha baada ya kumpoteza mume wake ambaye pia alikuwa meneja wake na baba watoto wake.

”Ninaposema bila Rene namaanisha, Rene atandelea kuwa sehemu ya maisha yangu kila siku” amesema Dion

Mwanamama huyo mwenye miaka 51 alipoulizwa kuhusu mahusiano mapya baada ya mume wake kufariki amesema kuwa ”Ninabahati  sana kuwa na watu wanaonizunguka na kunifanya nifurahi muda mwingi”.

Celine amesema hayo katika mahojiani na iHeartRADIO.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Septemba 21, 2019
Fatma Karume asimamishwa uwakili