Mwimabaji mkongwe, Celine Dion amekumbwa na majanga ya msiba wa watu wake wa karibu sana ndani ya siku mbili.

Siku mbili baada ya kutangazwa kwa kifo cha mume wa mwimbaji huyo, René Angélil aliyefariki Januari 14 mwaka huu kwa ugonjwa wa saratani, mdogo wa mwimbaji huyo aitwaye Daniel jana alitangazwa kuwa alifariki kutokana na ugonjwa huohuo akiwa na umri wa miaka 56.

Celine Dion na Mumewe René Angélil

Celine Dion na Mumewe René Angélil

Dada wa mwimbaji huyo aitwae Claudette aliiambia ‘Le Journal de Montreal’ kuwa kaka yake alikuwa anajua atafariki na alikuwa tayari. “Alikuwa anajua na hivi sasa hateseki tena,” alisema.

Baada ya kifo cha René Angélil, Celine Dion alieleza kuwa mumewe alikuwa amejiandaa na kifo hicho kwa sababu alikuwa anajua hakiepukiki. Rene alifariki akiwa na umri wa miaka 73.

TV 6, REdio 21 zikiwemo za CCM, Diallo na Lowassa zafungiwa
Gazeti la Mawio Lapigwa 'Kifungo cha Kudumu'