Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu bingwa Tanzania bara Simba SC, Barbara Gonzalez amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika CAF, Ahmad Ahmad kwenye makao makuu ya shirikisho hilo yaliyopo jijini Cairo, Misri.

Baada ya kukutana, Rais Ahmad amempongeza Barbara kwa kupata nafasi hiyo kubwa, lakini pia kumtaka kuitumia vyema ili kuonesha kwamba anaimudu kazi hiyo ambapo itakuwa ni moja ya njia ya kuhamasisha wanawake wengine kushika nafasi za juu za uongozi wa soka.

Kwa upande wake Barbara amemshukuru Rais Ahmad na CAF kwa mapokezi mazuri, lakini pia kuahidi kufanya kazi kwa bidii ili kusaidia kukuza soka la Afrika.

Wengine waliohudhuria kikao hicho ni Katibu Mkuu wa CAF, Abdelmounaïm Bah, Makamu Katibu Mkuu wa CAF, Anthony Baffoe na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, Mulamu Nghambi.

Kipaumbele cha wizara ya afya katika nafasi za ajira
Suarez achomoka kilaini, Barca wakubali