Aliyewahi kuwa Kiungo wa Hispana Cesc Fabregas anaamini kuwa, usajili uliofanywa na Arsenal, utawafanya kuwa imara hata kuwania taji la Premier League msimu huu, huku akieleza kwamba, Chelsea itawachukua muda mpaka kukaa sawa.

Fabregas aliwahi kuzichezea timu za Arsenal na Chelsea kwa nyakati tofauti.

Arsenal wametumia zaidi ya Pauni 200m kipindi hiki cha usajili wakiwasajili Declan Rice, Kai Havertz, Jurrien Timber na David Raya.

Kiungo huyo raia wa Hispania, anaamini uwekezaji ambao wamefanya Arsenal utawabeba kwa kiasi kikubwa na kutoa ushindani kwa Manchester City.

Fabregas alisema: “Arsenal watapanbania tena taji la Premier League kwa asilimia 100. Hii Arsenal ya sasa naona ni imara kuliko ya msimu uliopita, nafikiria wataenda kuwasumbua Man City.

“Kama wanataka kushinda taji itabidi wapambane kweli kwani hata wapinzani wao nao hawatabweteka, bidii zaidi ya msimu uliopita ndiyo itawabeba.”

Kiungo huyo alifunguka kuhusiana na biashara nzuri ambayo walifanya Chelsea.

“Naona kile wanachojaribu kukifanya wanajenga timu mpya tena ya vijana wadogo, imara na yenye nguvu ambayo itawachukua muda kuwa bora na hata kuwania taji la Premier League.

Wachezaji ambao wamesajiliwa hapo ni wale bora, kilichobaki ni kuwaweka pamoja ili kuendana na ligi na mambo yatakuwa mazuri.

“Mfano mzuri Enzo Fernandez tayari amekaa pale nusu msimu, hivyo atakuwa msaada, Moises Caicedo ni mchezaji bora mwenye nguvu na anaweza kupambana,” alimaliza.

Iddy Nado akiri mambo magumu Ligi Kuu Bara
Kramo, Inonga mambo safi Simba SC