Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kuwa kimejipanga kupata viongozi makini na wasiorubunika kwa tamaa za fedha kutoka Chama cha Mapinduzi(CCM), katika uchaguzi wa kanda ya ziwa unaotarajiwa kufanyika februari mwaka huu.
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa chadema kanda ya ziwa Peter Mekele, amesema kuwa maandalizi ya uchaguzi yanaendelea vizuri na tayari wanachama wameonesha nia ya kugombea nafasi mbalimbali.
“Miaka 20 iliyopita tangu chadema inaanzishwa viongozi wengi waliokuwa wanachaguliwa kwa sababu wanajua kuzungumza na ni wanaharakati anaeonekana kuipinga serikali, lakini tumeona watu hao ni wepesi sana kurubuniwa”amesema Mekele.
Aidha, Mekele amesema kuwa chadema kimejipanga kurudi nyuma kuhakikisha kinawaibua viongozi kutoka shuleni na vyuoni ili kuwapata viongozi wenye misimamo na makini katika kukitetea chama hicho.