Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kuwa kina uhakika wa kushinda uchaguzi mdogo wa ubunge wa jimbo la Singida Kaskazini ambalo Bunge lilitangaza jana kuwa liko wazi baada ya aliyekuwa Mbunge wake kujiuzulu mapema wiki hii.

Hayo yamesemwa na Afisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene, ambapo amesema kuwa wanauhakika watashinda katika uchaguzi huo mdogo, hivyo watamtangaza mgombea wake, baada ya NEC kutangaza kuhusu uchaguzi huo.

“Tutamtangaza mgombea wetu ambaye tutamsimamisha kwenye uchaguzi huo mdogo na tunaamini tutakayemsimamisha lazima atashinda kwa kuwa chama chetu kinakubarika kwa wananchi,”amesema Makene.

Aidha kwa upande wake Mkurugenzi wa NEC,, Ramadhani Kailima amesema kuwa muda ukifika watatangaza tarehe rasimi ya kuanza mchakato wa uchaguzi huo mdogo ili kuweza kuziba pengo lililopo.

Hata hivyo, Taarifa ya Bunge iliyotolewa jana na Spika wa Bunge imesema kuwa ameandika barua hiyo kwa mujibu wa kifungu 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi (Sura ya 343, ya mwaka 2015) kinachoelekeza kwamba, pale ambapo Mbunge atajiuzulu, atakufa au sababu nyingine yeyote tofauti na zilizoainishwa katika kifungu cha 113, Spika atamjulisha Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kutangaza kwenye Gazeti la Serikali kwamba kiti hicho cha Ubunge kiko wazi

Nadal ajitoa katika michuano ya Paris Masters
Kivumbi cha uchaguzi kutimka jimboni kwa Nyalandu