Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) upande wa Zanzibar, kimesema kuwa hakihusiki na maandamano yaliyo pangwa kufanyika tar. 26 mwezi huu.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja, Idrissa Jumbe Mkila alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo viongozi wa chama.
“Hatuna taarifa wala hatuna nafasi ya kujiingiza katika masuala kama hayo ambayo hayana tija kwa nchi yetu, kama chama sisi tumesha toa taarifa kwa viongozi wetu na wanachama waendelee na shughuli zao,”amesema Mkila
Kwa upande wake, Kamishna wa jeshi la polisi Zanzibar, Mohamed Haji Hassan amesema kuwa vikosi vyake vyote vya ulinzi viko vizuri, na kuonya kuwa yeyote atakayejihusisha na maandamano atachukuliwa hatua kali.
-
John Heche kupandishwa kizimbani
-
Subirini kwanza JPM atunyooshe- Polepole
-
Video: Polepole amlipua Zitto, amtaka aache kudanganya umma