Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeitaka tume ya taifa ya Uchaguzi NEC kuitaja kampuni iliyopewa tenda ya kuchapisha karatasi za kupigia kura na kueleza umma wazi mchakato wa ununuzi ulivyopitiwa.

Akizungumza katika makao makuu ya Chama hicho jijini Dar es Salaam Katibu mkuu wa Chama hicho Taifa John Mnyika amesema licha ya Tume kuitisha kikao cha kwanza tarehe 8 Oktoba, kamati ya zabuni ya manunuzi inayohusisha vyama vya siasa haijaelezwa jina la kampuni iliyopewa zabuni licha ya uwepo wa majina mawili ambayo yametajwa.

Adha Mnyika ameitaka tume kuweka wazi mfumo wa ujumlishaji wa matokeoya uchaguzi mkuu huku akisema wamepeleka malalamiko kwa tume baada ya mgombea wa CCM kukiuka taratibu za uchaguzi na kufanya kampeni yake binafsi na wagombea wengine katika kazi ya serikali wakati wa uzinduzi wa kituo cha mabasi cha Mbezi.

Wakati huohuo, Mnyika amemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, kumchukulia hatua OCD wa wilaya ya Hai na si kuunda kamati ya kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chama hicho na mgombea wa jimbo la Hai Freeman Aikaeli Mbowe kwa kumtakia mgombea huyo kuwa hatashinda uchaguzi.

Ufanyaji wa mazoezi kupunguza magonjwa yasiyoambukiza
Lissu amaliza adhabu, arejea kwenye kampeni