Chama cha demokrasia na maendeleo kupitia kwa afisa habari wake  Tumaini Makene kimekanusha vikali kuhsiana na video zinzo zagaa mitandaoni zikionyesha mwanamke mmoja aliyeshika silaha za jadi mikononi mwake,panga,upinde na mishale huku akiwa amevalia nguo zenye rangi na nembo ya chadema.

Makene kupitia taarifa aliyoitoa katika tovuti ya chama hicho amesema mtu huyo ameonekana pia akifanya mazoezi huku nyuma yake kukiwa na bendera ya chadema,aidha aliongeza kuwa picha hizo zinamuonyesha mtu huyo akijiandaa kwa shari.

”Tungependa kutaarifu umma kuwa picha hizo zisihusishwe kwa namna yoyote ile na Operesheni UKUTA na maandalizi ya Septemba 1 kwa ajili ya mikutano ya hadhara na maandamano ya amani kwa mujibu wa Sheria za Nchi, ambayo inatarajiwa kufanyika katika kutimiza wajibu na haki za kikatiba za Watanzania”Alisema Makene.
Hata hivyo kupitia taarifa hiyo makene alisema Chama kinalaani vikali matumizi ya nembo za chama yaliyofanywa na watu hao kwa namna inayoashiria shari na vurugu huku ikihusishwa na Operesheni UKUTA ya Septemba 1. Waliozipiga na kuzisambaza mitandaoni.

Mhariri Mkuu BAKITA Awaasa Watanzania Kutunza Lugha Za Asili Ili Kuboresha Kiswahili
Mkapa;Kila Mmoja Ni Zawadi Kwa Mwenzie,Awakutanisha Lowassa Na Rais Magufuli Katika Jubilei Ya Miaka 50 Ya Ndoa Yake