Mawakala na viongozi wa CHADEMA waliokamatwa wakati wa uchaguzi mdogo wa marudio Novemba 26 wameshindwa kufikishwa mahakamani leo kwa kukosa polisi wa kuwasindikiza.

Hayo yamesemwa na Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche ambapo amesema kuwa kutopelwekwa mahakamani kwa watu hao ni muendelezo wa kucheza na haki za binadamu.

“Mawakala na viongozi wetu waliokamatwa tarehe 26 na kunyimwa dhamana hapa Maswa mkoani Simiyu wameshindwa kuletwa mahakamani, ambapo ndio ilikua siku ya kesi,”amesema Heche

Hata hivyo, Heche amesema kuwa kukosekana kwa polisi wa kuwasindikiza mahakamani watu hao walionyimwa dhamana ni muendelezo wa kuminya haki za binadamu.

Magazeti ya Tanzania leo Desemba 8, 2017
JPM atinga mkoani Dodoma