Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kimeitaka Serikali kufanya Mabadiliko katika kanuni ya kikokotoo ya mafao ya mwaka 2018 yaliyopendekezwa katika kiwango cha asilimia 25, ili angalau kuwalipa wafanyakazi asilimia 50.

Akizungumza na Waandishi wa habari hii leo Febuari 12 2023 Jijini Dodoma, Mjumbe wa Kamati kuu ya Chama hicho, John Heche amesema hiyo ni dhuluma na wao kama chama cha Wananchi hawatakubali.

Amesema, “hizo fedha ni fedha za Wastaafu na sio za Serikaki,  na kama mnakumbuka Kinacholeta Ugomvi wote huu ni hii mifuko ya hifadhi ya Jamii Serikali wameikopa fedha ndio  wakajenga pale Udom chuo kikuu, wamekopa wakawekeza kwenye miradi mingi na fedha nyingine zimeibiwa.”

Mjumbe wa Kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo -CHADEMA, John Heche.

Heche ameongeza kuwa, Serikali inataka kuvunja  makubaliano ya awali ambayo walikuwa wameweka na Wafanyakazi, na kwamba hatua hiyo imezua manung’uniko na inawaathiri wastaafu.

“Huwezi kuvunja makubaliano katikati ya Mchezo, Mtu alishaingia kazini alafu unakuja kuvunja makubaliano katikati na akati akishafanya kazi hili ni jambo ambalo haluwezekani hata kidogo,” amebainisha Heche.

Aidha, ameongeza kuwa baadhi ya Watu wamekopa kwa makubaliano ya kurejesha mara baada ya kupata malipo yao hivyo kitendo cha kuwabadilikia kinaleta tafsiri isiyo sahihi na kuathiri malengo waliyojiwekea maishani.

Nchi haina fedha, deni la Taifa laongezeka: Waziri
Wabunge ni Walafi na Wachoyo: Heche