Chadema wameendelea kuwahimiza wafuasi wake kuhakikisha hawaondoki katika vituo vya kupigia kura baada ya kupiga kura, licha ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwataka wananchi kurejea makwao baada tu ya kupiga kura.

Akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Bara, John Mnyika, alisema kuwa wafuasi wa Chadema wanapaswa kulinda vituo vya kura kwa kwa kukaa umbali usiopungua mita 100 kama sheria inavyoelekeza na sio kama inavyoelekezwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu, Damian Lubuva.

Akieleza umuhimu wa wananchi kubaki katika maeneo ya vituo vya kupiga kura, Mnyika alieleza kuwa inaweza kutokea wakala aliyeko kituoni akazidiwa nguvu na watu wenye mpango wa kuhujumu zoezi la kuhesabu kura kwa maslahi yao na hata kumfukuza msimamizi huyo, lakini hawataweza kufanya hivyo endapo wananchi watakuwa nje wakisubiri kuona matokeo yao yakibandikwa kwa haki.

Hivi karibuni, Jaji Damian Lubuva, aliwataka wananchi kuelekea majumbani kwao baada ya kupiga kura kwa kuwa hakuna kura hata moja itakayoibiwa.

Jaji Lubuva alisisitiza kuwa Chadema wanapaswa kuwaweka wasimamizi wanaowaamini ambao watakuwa wawakilishi wao wakati wa kuhesabu kura kwa kuwa wananchi kubaki kwenye vituo vya kupigia kura kunaweza kuleta vurugu na uvunjifu wa amani.

Amshtaki Mbunge Wa Chadema Kwa Magufuli Kwa Tuhuma Za Kubakwa na Viongozi wa CCM
Kingunge Aitosa Rasmi CCM Na Kujiunga Na 'Mabadiliko', Hotuba Yote Hapa