Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar), Salum Mwalimu amesema kwamba matukio yanayoendelea kutokea  hayawezi kuwaziba midomo au kusimamisha kazi zao bali yanazidi kuwaimarisha zaidi kisiasa.

Ameyasema jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa chama hicho hakijafungwa mdomo tangu tukio la kupigwa risasi kwa mwanasheria wa chama hicho, Tundu Lissu.

Amesema kuwa tukio la kushambuliwa kwa kiongozi wao hakujafanya chama hicho kushindwa kuendelea na shughuli za chama na badala yake wanaendelea kuimarisha chama.

“Tupo kwenye vikao vizito vya kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye uchaguzi mdogo uliotangazwa. tukio hili la Lissu halijafanya shughuli za chama zisimame, Shughuli zinaendelea kama kawaida. Mikoani na makao makuu ya chama mambo yetu yanaenda kama awali,”zmesemz Salum Mwalimu

Hata hivyo, kuhusu maendeleo ya Mbunge wa Singida Mashariki, amesema kuwa watatoa taarifa siku chache zijazo, hivyo amewataka wanachama wa chama hicho kuwa watulivu.

Video: Sheikh Ponda ajitosa rasmi tukio la Lissu, Rais Magufuli, Aga Khan wazungumzia mambo 3
Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 12, 2017