Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetangaza kufanya mikutano ya hadhara nchi nzima Septemba Mosi mwaka huu.
 Uamuzi huyo wa Chadema umetangazwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mapema leo akielezea baadhi ya maamuzi yaliyofikiwa katika Mkutano wa Kamati Kuu ya chama hicho uliofanyika wiki hii.
Mbowe aliwataka viongozi wa wakuu wa chama hicho, wabunge, na madiwani wote wa chama hicho kuandaa mikutano ya ndani ya chama kwa ngazi zote ili kufanya maandalizi ya Septemba Mosi.
Aidha, Mwenyekiti huyo amesema Kamati Kuu imepinga vikali kitendo cha Polisi kupiga marufuku mikutano ya hadhara ya kisiasa nchi nzima hadi mwaka 2020 kwakuwa tangazo hilo ni kinyume cha matakwa ya katiba.
Amesema kuwa mkutano huo utakuwa ni sehemu ya kampeni maalum waliyoiita Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania (UKUTA).
“Operation UKUTA umeazimiwa kwaajili ya kila mtanzania anaeona haki na demokrasia ni jambo la msingi,” alisema Mbowe.
Kamati Kuu ya Chadema ilikutana kwa dharura wiki hii kwa lengo la kujadili hali ya kisiasa nchini, kubwa likiwa kuzuiwa kwa mikutano ya hadhara ya kisiasa.

Sheria Ya Wachezaji Wanne Wa Akiba Kutumika England
BreakingNews: Mahakama Yatoa Hukumu Mauaji Ya Mwangosi