Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetetea hatua ya Mbunge wake wa Jimbo la Ndanda, Cecil Mwambe kuingia na ilani ya Chama Cha Mapinduzi bungeni kwa kile ilichokisema kuwa ni jambo la kawaida.
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano wa Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema amewataka wananchi na wafuasi wa chama hicho wasishangae kwani chama hicho kinawahamasisha wabunge wake kusoma ilani ya CCM ili kujua namna gani ambavyo chama hicho tawala kinatekeleza Ilani yake.
“Ni jambo la kawaida sana, sababu sisi kama chama tunahamasisha wabunge wetu kusoma, ndio maana huyo huyo Mwambe wiki iliyopita ulimuona anampa sera mbadala za Chama moja ya mawaziri Bungeni,”amesema Mrema
Aidha, amesema kuwa kuingia na ilani ya Chama Cha Mapinduzi sio tatizo kwa sababu hata ofisini kao ukienda utakutana na ilani ya CCM kwa hiyo kama angekuwa na nia ya kuhama chama, basi angehama kimya kimya kama wanavyofanya wengine.
-
Chadema yawakaanga Kubenea na mwenzie
-
Sijawahi kuomba kujiunga CCM, Polepole ni muongo- Komu
-
Gekul, Millya, Mkundi, na Ryoba waula tena CCM
Leo Novemba 14, 2018 akiongoza vikao vya bunge, Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson amesema kuwa, Cecil Mwambe anasoma sana ilani ya Chama Cha Mapinduzi, siku hizi baada ya kugundua ina mambo mazuri sana.