Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kaskazini, Aman Gorugwa amesema kuwa hawaridhiki na mazingira ya madiwani wao saba kujivua nafasi zao za madaraka.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa sakata hilo wameamua kulifikisha kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( Takukuru) na Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma ili iweze kutafutiwa ufumbuzi.

Amesema kuwa haoni sababu yeyote ya msingi ya viongozi hao kujivua nafasi zao ndio maana wamefikia hatua hiyo ya kulifikisha jambo hilo mbele ya vyombo hivyo ili viweze kulichunguza kiundani zaidi.

“Wale wanaotaka kuondoka waondoke sasa, watakaotaka washuke washuke tu, tunaamini CCM hawatakaa milele madarakani kwakuwa mambo yanabadilika kila kukicha,”amesema Gorugwa.

Hata hivyo, amewataka wafuasi wa Chama hicho kutotafuta mchawi bali wafukuze wasaliti waliomo ndani ili waweze kukijenga na kuimarisha utendaji kazi wake katika kutoa upinzani uliokuwa imara.

Hivi karibuni madiwani saba wamejivua uanachama wa chama hicho katika kata za Abureni, Ngabobo, Muriet, Legaruki, Makiba, Maroroni na mwingine ni wa diwani wa viti maalumu kutoka chama hicho.

 

 

Video: Makonda kugawa Kompyuta kwa Halmashauri zote Dar
Rais wa Brazil kikaangoni, Bunge lamkingia kifua