Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemuandikia barua Kaimu Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma kulalamikia kitendo cha mahakama nchini kuwanyima dhamana wanachama wake pindi wanapofikishwa mahakamani.
Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Prof. Abdallah Safari mapema hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akiwasilisha azimio hilo kwenye Kamati Kuu ya chama hicho.
Amesema kuwa katika barua hiyo wamebainisha kesi tano za viongozi na wanachama wa chadema ambao wameyimwa au kucheleweshewa dhamana zao katika mahakama mbalimbali.
“Hivi ndivyo vitu ambavyo Kaimu Jaji Mkuu anatakiwa avifahamu, yeye ndiye mhusika Mkuu wa uhuru wa mahakama, ninaamini kwamba nitalifanyia kazi suala hili ili viongozi wetu na wafuasi wapate haki yao ya msingi,”amesema Prof. Safari.
Hata hivyo, amezitaja kesi hizo kuwa ni pamoja na inayomkabili Katibu Mkuu wa chama hicho Vincent Mashinji, nyingine inamkabili Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu, na zingine kote nchini zinazo wakabili viongozi na wafuasi mbalimbali wa chama hicho.