Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeibuka na kudai kuwa aliyekuwa mbunge wa jimbo la Ukonga kupitia chama hicho, Mwita Waitara alikuwa ni mzigo.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Kinondoni, Makongoro Mahanga mara baada ya aliyekuwa Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara kupitia chama hicho kujiuzuru nafasi yake na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mahanga amesema kuwa sababu alizozitoa Waitara wakati anaondoka ni uongo, sababu kubwa ni kwamba alikuwa anakaribia kufukuzwa na kunyang’anya nafasi zote za kichama
Aidha, ameongeza kuwa Waitara alishapewa barua za kufukuzwa tayari na kuondoka kwake wametua mzigo mkubwa huku wakiwaonea huruma CCM kwa kuchukua mzigo huo
Hata hivyo, Mwita Waitara alijiunga CCM jana na kudai kuwa baadhi ya sababu ni kutofautiana na Mwenyekiti, Freeman Mbowe baada ya kuhoji kuhusu uchaguzi wa Mwenyekiti na masuala ya rukuzu.