Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mkoani mbeya umekana madai ya mkazi wa Kata ya Ruanda Nzowe, Amon Mwakyambiki anayedai chadema haijamlipa shilingi milioni moja za fidia baada ya wafuasi wake kumvunjia paa la nyumba yake katika kampeni za mgombea urais Edward Lowassa 2015.

Aidha, Mwenyekiti wa Chadema mkoani Mbeya Joseph China, amesema kuwa madai ya Mwakyambiki ameyasikia kwenye magazeti, lakini hayajafika ofisini kwake kimaandishi na kwamba anashangaa kusikia suala hilo.

“Sisi ofisini kwetu tangu Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015, hatujampokea mtu yeyote aliyewasilisha malalamiko  juu ya uharibifu wa mali zake, hivyo tunashangaa kuelezwa kwamba uongozi wa chadema umeshindwa kumlipa fidia,”amesema Joseph.

Aidha wiki lilyopita Mwakyambiki litoa malalamiko yake kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla, aliyekuwa akisikiliza kero za wananchi, kwamba chadema haijamlipa shilingi milioni moja walizomuahidi baada ya wafuasi wa chama hicho kuvunja paa la nyumba yake.

Hata hivyo Mwakyambiki baada ya kuvunjiwa paa lake na wafuasi hao alikwenda kutoa taarifa kwa Mstahiki Meya wa jiji, David Mwasilindi ambaye alimuahidi kumlipa kiasi hicho cha pesa lakini mpaka sasa hajatimiza ahadi yake

Azam FC Wampata Mrithi Wa Zeben Hernandez
#HapoKale