Madiwani watatu kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoani Iringa wamejiuzuru nafasi zao na kukihama chama hicho kwa kile wanachodai kuwa viongozi wao ngazi za juu wametawaliwa na rushwa na ubaguzi dhidi ya baadhi ya madiwani.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake, diwani wa Kata ya Kitwiru, Baraka Kimata amesema kuwa wameamua kufanya maamuzi hayo magumu ili hali wanatambua kuwa wapo watu watachukizwa na maamuzi hayo lakini hawana jinsi kwa kuwa wamevumilia mambo mengi ndani ya chama hicho.
“Najua wapo watu wataumia kutokana na maamuzi haya lakini sina jinsi imebidi nifanye maamuzi magumu kwani kuna wakati watu mnafanya vikao hafikii maamuzi kutokana na mabishano mpaka muda mwingine mnatishiana maisha sasa tunaendelea kutafakari hichi chama ambacho kimewaaminisha Watanzania kuwa chama mbadala kikachukua dola kitawaletea Watanzania nini,”amesema Kimata
-
Zitto Kabwe: Hatukutaka mnunue ndege hovyo hovyo
-
Hamad Rashid: Wanasiasa acheni kutoa kauli za kichochezi
-
Lissu akamatwa na Jeshi la Polisi Dar
Hata hivyo, ameongeza kuwa kuna mambo makubwa ambayo chama hicho kinayafanya bila mpangilio wowote kwani wamekuwa wakitanguliza rushwa mbele kuliko maslahi ya Watanzania