Mwenyekiti wa Wilaya ya Siha (CHADEMA), na Diwani wa Kata ya Gararagua ametangaza kujivua nafasi zake zote za uongozi ndani ya Chama hicho na kutangaza anahamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuungana na Rais Dkt. Magufuli kulinda rasilimali za nchi.

Zakaria Lazaro Lukumay amesema kuwa anaamini kwamba CCM ndicho chama pekee ambacho kinagusa maisha ya watanzania hivyo ameamua kujiunga ili kutetea, kulinda, na kusimamia rasilimali za nchi ikiwa ni pamoja na kupiga vita ufisadi, rushwa na mambo mengine yanayofanana na hayo.

Katika taarifa yake aliyoituma kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha,  Lukumay amesema kuwa anaamini katika maamuzi yake aliyoyafanya atakuwa huru kuungana na Mh. Rais dkt. Magufuli katika kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015.

Lissu afanya muujiza, asimama kwa mara ya kwanza
Magazeti ya Tanzania leo Desemba 27, 2017